SERA YA FARAGHA NA ILANI YA KISHERIA

Sera ya Faragha

Sera hii ya faragha inahusu haswa tovuti hii ya oxforddictionaries.com ("Tovuti") na tanzu zake na inasimamia utumiaji wako wa Tovuti hii na tanzu zake.

Oxford University Press ("OUP", "tu", "sisi" au "-etu") inajizatiti katika kulinda faragha yako mtandaoni. Sera hii ya faragha inaeleza jinsi tutakavyofanya hivi. Tutarekebisha sera hii ya faragha kutokana na maoni tunayoyapokea kwa hivyo angalia toleo lile la kisasa zaidi. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera hii ya faragha, tafadhali wasiliana nasi.

Kwa kutumia Tovuti hii, unakubali vitendo vinavyofafanuliwa katika taarifa hii.


Je, ni maelezo ya aina gani tukusanyayo na huwa tunayatumia vipi?

Unapotembelea Tovuti hii, OUP huenda ikusanye maelezo na takwimu zilizo na maelezo yako yanayokutambulisha. Maelezo yaliyokusanywa huenda yajumuishe maelezo yanayohusu mwenendo na sehemu ulizofungua kwenye Tovuti. Maelezo haya huturuhusu kufanya utafiti wa ndani kuhusu yanayowavutia watumiaji wetu, demografia na mienendo ili tuweze kuelewa vyema, na mwishowe, tuweze kutoa maelezo, bidhaa na huduma bora kwako na kwa wateja wengine.

Ukijisajili kama mtumiaji wa Tovuti hii au ukiomba maelezo zaidi kuhusu Tovuti hii, huwa tunaomba jina lako, anwani ya barua pepe, anwani ya posta, na maelezo mengine muhimu ya kibinafsi. Maelezo ya kibinafsi yaliyowasilishwa kwa namna hii huongezwa kwenye hifadhidata ya kudhibiti ufikiaji, inayopangishwa na kampuni ya upangishaji ya mhusika asiyehusika moja kwa moja, na kwenye hifadhidata za wateja wetu kwenye OUP na/au ya washirika wetu. Maelezo haya yatasasishwa ukitujuza kuhusu mabadiliko yoyote.

Ikiwa wewe ni mtumiaji aliyesajiliwa, maelezo yako ya kibinafsi yatatumiwa kutuwezesha kuthibitisha kuwa wewe ni mtumiaji aliyesajiliwa na kukufikishia makala yoyote yaliyozuiwa na kukuwezesha utumie Tovuti hii.

Ukijiandikisha kupokea vijarida, tutakuomba anwani yako ya barua pepe na jina lako na maelezo haya yataongezwa kwenye hifadhidata ya wateja wetu.

Ukipakia makala kwenye Tovuti, huenda tuonyeshe taarifu zinazokuhusu (yaani, jina na nchi yako) kwenye Tovuti.

Tunaweza kutumia maelezo yaliyoko kwenye hifadhidata ya wateja wetu kukutumia kielektroniki au vinginevyo, maelezo kutuhusu, kuhusu washirika wetu, kuhusu bidhaa na huduma zetu, na kuhusu bidhaa na huduma za washirika wetu ambazo tunafikiri kuwa huenda zikuvutie.

Huwa tunaomba maelezo ya kibinafsi (kama vile jina lako, anwani ya barua pepe na maelezo mengine ya mawasiliano) kutoka kwako unapowasiliana nasi kuhusu maswali ya usimamizi wa akaunti ya mtumiaji aliyesajiliwa, matatizo ya kiufundi, kutoa maoni kwenye Tovuti, au unapoomba maelezo kuhusu jinsi ya kutumia bidhaa na/au huduma zinazopatikana kwenye Tovuti. Maelezo ya kibinafsi uliyoyawasilisha kupitia ukurasa wa "wasiliana nasi" hayatajumuishwa kwenye hifadhidata za wateja wetu na huwa tunayaomba ili tuweze kujibu swali lako. Huenda tukusanye kiujumla takwimu kuhusu aina za maswali yaliyowasilishwa kwetu kupitia ukurasa wa "wasiliana nasi" ili tuweze kufuatilia Tovuti kifanisi na tuboreshe viwango vya huduma.

Ikiwa umewahi kuomba maelezo hapo awali au kujisajili kwenye Tovuti (na hatimaye ukafunga akaunti yako ya mtumiaji) na hutaki tuhifadhi maelezo kukuhusu, tafadhali wasiliana nasi  na tutaondoa maelezo hayo kwenye hifadhidata za wateja wetu. Tunahitaji kuhifadhi maelezo kuhusu watumiaji wa sasa waliosajiliwa ili tukuruhusu ufikie makala yaliyozuiwa na uweze kutumia Tovuti hii.

Unaweza kutuarifu kuwa hutaki tuwasiliane nawe au hutaki tuwasiliane nawe kupitia njia fulani iliyotajwa. Ikiwa wewe hutumia zaidi ya anwani moja ya barua pepe kuwasiliana nasi, tafadhali  tuarifu kuhusu kila anwani ya barua pepe uitumiayo.


Je, huwa tunashiriki maelezo wakati gani?
Huwa hatuuzi maelezo yako ya kibinafsi kwa watu wasiohusika moja kwa moja.

Huwa tunashiriki maelezo yako ndani ya OUP. Pia, huwa tunashiriki maelezo yako na washirika, watoa leseni na wasambazaji wetu, inayotusaidia katika kuhakikisha kuwa Tovuti hii inapatikana kwako (k.mf. msambazaji mpangishaji wetu).

Baadhi ya tovuti za wahusika wa kando zinafikiwa  kutoka Tovuti yetu. Ukitembelea yoyote kati ya tovuti hizo, huenda wakusanye maelezo. Hatudhibiti tovuti kama hizo na hazishughulikiwi na sera hii ya faragha. Tovuti hizi huenda ziwe na sera zao za faragha na hatuwajibikii sera hizo. Tafadhali chunguza sera hizo kabla uwasilishe data yoyote ya kibinafsi kwenye tovuti hizi za wahusika wa nje.

Tukiamini kwamba utumiaji wako wa Tovuti hii unakiuka sheria au unawakosea wengine, tuna haki ya kufichua kwa wasiohusika moja kwa moja, maelezo yanayokuhusu tuliyoyapata kupitia Tovuti kwa kiasi kinachohitajika kwa maoni yetu ili kuzuia, kufidia au ili hatua ichukuliwe kufuatia mwenendo huu.

Pia, tunaweza kufichua au kushiriki data yako ya kibinafsi ili tuweze kutimiza wajibu wowote wa kisheria; ili tuweze kutekeleza au kutumia leseni au mikataba yoyote nawe; au kulinda haki, mali, au usalama wa OUP, wafanyakazi, washirika, watoa leseni wetu, wasambazaji, na/au wateja wetu. Hii inajumuisha ubadlishanaji wa maelezo na kampuni na mashirika mengine kwa madhumuni ya ulinzi kutokana na ulaghai na upunguzaji hatari ya mkopo.

Ikiwa sehemu yoyote ya biashara yetu (ikiwa ni pamoja na zile za washirika wetu) imeuzwa au kujumuishwa na biashara nyingine, maelezo yako yanaweza kufichuliwa kwa washauri wetu na wanunuzi wowote watarajiwa na washauri wao.


Utumiaji wa kuki

OUP hutumia "kuki" na teknolojia zingine kwenye Tovuti. Sheria na masharti yanayosimamia utumiaji wa OUP wa "kuki" na teknolojia zingine za aina hii kwenye Tovuti yamefafanuliwa katika Sera ya Kuki ya OUP. Sera hii ya Kuki ipo katika lugha ya Kiingereza. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa ungependa kuipokea katika lugha nyingine.

Kwa kutumia Tovuti hii, unakubali kuwajibishwa kisheria na masharti ya Sera yetu ya Kuki.


Usalama

Baadhi ya maelezo yako ya kibinafsi yamehifadhiwa katika kituo cha data kinachosimamiwa na kampuni ya upangishaji ya mhusika wa kando. Kituo hiki cha data kinachosimamiwa na kampuni ya upangishaji ya mhusika wetu wa kando kimeundwa haswa kuwa salama kihalisi na kuingiza wafanyakazi walioidhinishwa pekee, ambao wamewajibishwa kimkataba kuweka siri data yetu yote.

Mtu anaweza kufikia hifadhidata za wateja wetu 'kwa misingi ya kutaka kujua' pekee.

Maelezo tunayokusanya kutoka kwako yanaweza kuhamishwa hadi, na kuhifadhiwa, pahali palipo nje ya Eneo la Kiuchumi la Uropa (EEA). Pia, yanaweza kuchakatwa na wafanyakazi wanaoendesha shughuli nje ya EEA wanaotufanyia kazi, washirika wetu au kwa mmoja wa wasambazaji wetu. Hata hivyo, tumechukua hatua zilizofafanuliwa hapo juu ili tujaribu kuboresha usalama wa maelezo yako. Kwa kutumia Tovuti hii, unakubali mahamisho haya.


Kusasisha Maelezo Yako
Maelezo yoyoye uliyoyatoa kwa OUP yakibadilika k.mf. ukibadilisha anwani yako ya barua pepe, tafadhali tujuze kuhusu maelezo sahihi kwa kuwasiliana nasi.


Mabadiliko kwa Sera yetu ya Faragha
Tuna haki ya kufanya mabadiliko kwenye sera hii ya faragha. Mabadiliko yoyote tunayoweza kufanya katika sera hii ya faragha yatachapishwa kwenye ukurasa huu na, ikihitajika, utaarifiwa kupitia barua pepe.


Lugha
Sera hii ya faragha imeandikwa katika lugha ya Kiingereza. Ikiwa sera hii ya faragha imetafsiriwa katika lugha nyingine yoyote, toleo lile la lugha ya Kiingreza ndilo litakalofuatwa.


Sheria Inayoongoza
Unakubali kwamba sera hii ya faragha itaongoza kwa kuzingatia sheria za na mahakama zilizoko Uingereza na Wales.


Ilani ya Kisheria
Ilani hii ya kisheria inahusu haswa tovuti hii ya oxforddictionaries.com ("Tovuti") na tanzu zake na inasimamia utumiaji wako wa Tovuti hii na tanzu zake. Kwa kutumia Tovuti hii, unakubali vitendo vilivyofafanuliwa katika taarifa hii.

Unaweza kufikia sehemu fulani za Tovuti bila kujisajili au bila kutoa maelezo yako kwa Oxford University Press ("OUP", "tu", "sisi" au "-etu").

Kwa vile maelezo yaliyoko kwenye Tovuti huenda yawe ambayo hayajakamilika, yaliyopitwa na wakati au yasiyo sahihi na huenda yawe na makosa ya kiufundi au ya kimaandishi, OUP ina haki ya kusasisha Tovuti hii kwa kuhusisha uamuzi wetu pekee. Kwa hivyo, maelezo ya aina hii yanaweza kubadilishwa au kusasishwa bila ilani.

Tuna haki ya kufanya mabadiliko katika ilani hii ya kisheria. Mabadiliko yoyote tunayoweza kufanya katika ilani hii ya kisheria yatachapishwa kwenye ukurasa huu na, panapofaa, tutakuarifu kupitia barua pepe pia. Masharti fulani ya ilani hii ya kisheria huenda yatawaliwe na masharti na ilani za kisheria zilizoonyeshwa wazi zinazopatikana katika kurasa mahususi za Tovuti.


Majina ya Watumiaji na Nywila
Pale ambapo umejisajili kwenye Tovuti na umepewa jina la mtumiaji pamoja na nywila, unakubali kutopeana jina lako la mtumiaji na/au nywila yako kwa yeyote yule. Ikiwa jina lako la mtumiaji na/au nywila yako imefichuliwa kwa yeyote yule, unakubali kutuarifu haraka iwezekanavyo kuhusu kufichuliwa huku ili OUP ichukue hatua mwafaka za kiusalama na ikupe jina jipya la mtumiaji na nywila mpya.


Utumiaji wa makala ya Tovuti
Unaruhusiwa ku:

1.  Tafuta, kuona, nyofoa, na kuonyesha sehemu fulani za makala ya Tovuti;

2.    hifadhi kielektroniki sehemu fulani za makala ya Tovuti;

3.    na/au kuchapisha nakala moja moja ya kila sehemu ya makala ya Tovuti unayoruhusiwa kuchapisha

Katika kila hali, kwa kuzingatia onyo za kipekee zinazopatikana katika kurasa mahususi za Tovuti. Hupaswi kuondoa wala kubadilisha ilani za hakimiliki au njia yoyote ya utambulisho au taarifa za kujiondoa hatiani kama zilivyo kwenye Tovuti; pia hupaswi kuchapisha nakala nyingi au kuwa na nakala nyingi za kielektroniki za sehemu za makala yaliyozuiwa kwa madhumuni yoyote isipokuwa kama inavyoruhusiwa kisheria au ilivyoidhinishwa na OUP; hupaswi kuonyesha au kusambaza sehemu yoyote ya data husika kwenye mtandao wowote wa kielektroniki, ikiwemo bali sio tu Intaneti na Mtandao wa Dunia Nzima; hupaswi kumruhusu yeyote afikie au atumie data hiyo; na/au hupaswi kutumia au kumruhusu yeyote atumie yote au sehemu yoyote ya data husika kwa shughuli zozote za kibiashara.

Ukijiandikisha kupokea vijarida au ukijiandikisha kupokea masasisho ya makala, unapaswa kutumia data uliyotumiwa kwa matumizi yasiyo ya kibiashara pekee. Hupaswi:

1.    kuondoa wala kubadilisha ilani za hakimiliki au njia yoyote ya utambulisho au taarifa za kujiondoa hatiani kama zilivyo kwenye data uliyotumiwa;

2.    kuchapisha nakala nyingi au kuwa na nakala nyingi za kielektroniki za sehemu za data hiyo kwa madhumuni yoyote isipokuwa kama inavyoruhusiwa kisheria au ilivyoidhinishwa na OUP;

3.    kuonyesha au kusambaza sehemu yoyote ya data husika kwenye mtandao wowote wa kielektroniki, ikiwemo bali sio tu Intaneti na Mtandao wa Dunia Nzima;

4.    kumruhusu yeyote afikie au atumie data hiyo; na/au

5.    kutumia yote au sehemu yoyote ya data husika kwa shughuli zozote za kibiashara.


Haki za Mali ya Kiakili
Sisi na/au watoa leseni wetu ndio wamiliki wa haki zote za mali ya kiakili kwenye Tovuti, na Tovuti na data iliyoko kwenye Tovuti zinalindwa na sheria za mali ya kiakili ulimwenguni ikiwa ni pamoja na sheria za hakimiliki na alama ya biashara. Kufuatia masharti ya ilani hii ya kisheria na mikataba mingine yoyote ya leseni kati yako na OUP, haki zote za aina hii zimehifadhiwa na hakuna data ambayo inapaswa kunakiliwa, kurekebishwa, kuchapishwa, kutangazwa au kusambazwa kwa namna yoyote bila idhini yetu ya awali iliyoandikwa. Oxford University Press, OUP, Oxford na/au majina yoyote yale ya bidhaa au huduma zozote zinazotolewa na Oxford University Press na yaliyotajwa kwenye Tovuti ni alama za biashara au alama za biashara zilizosajiliwa za Oxford University Press.

Licha ya yaliyotajwa hapo juu na inapotumika, hakimiliki katika kila mfano/picha iliyoko kwenye Tovuti inamilikiwa na mmiliki wa haki aliyetajwa kwenye dirisha la ‘Maelezo ya Picha’ la mfano/picha hiyo. Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna mfano/picha yoyote iliyoko kwenye Tovuti inayopaswa kunakiliwa, kurekebishwa, kuchapishwa au kutangazwa au kusambazwa kwa namna yoyote.


Viungo
Viungo vinavyokupeleka kwenye tovuti zingine vinatolewa na OUP na nia nzuri na kwa maelezo tu. OUP inajiondoa kwenye hatia inayotokana na data iliyoko kwenye tovuti yoyote iliyounganishwa kwa Tovuti hii.

Isitoshe, kiungo kinachokupeleka kwa tovuti isiyo ya OUP haimaanishi kuwa OUP inaidhinisha au inakubali wajibu utokanao na makala husika, au utumiaji, wa tovuti ya aina hii au bidhaa na/au huduma zinazotolewa kwenye tovuti ya aina hii. Ni jukumu lako kuchukua tahadhari ili uhakikishe kuwa unachochagua kukitumia hakina virusi, minyoo, trojani na vingine viharibifu.


Ufikiaji Huduma
Ingawa tunajizatiti kuhakikisha kuwa Tovuti hii inapatikana kwa kawaida kwa masaa 24 za siku, hatutawajibika ikiwa kwa sababu yoyote ile Tovuti hii haipatikani kwa wakati wowote au kwa kipindi chochote.

Ufikiaji Tovuti unaweza kusitishwa kwa mda mfupi na bila ilani ikiwa kuna hitilafu ya kimfumo, udumishaji au marekebisho au kwa sababu tusizoweza kudhibiti.


Makala kutoka kwa mtumizi
Sehemu fulani za Tovuti yetu huenda ziruhusu watumiaji wapakie makala yao wenyewe. Makala yaliyopakiwa na watumiaji hayawakilishi maoni ya OUP. Kwa kupakia makala kwenye Tovuti yetu, unakubali kufuata Maelekezo yetu. Unahakikisha kwamba makala ya aina hiyo yanafuata Maelekezo hayo na kuwa una haki zote zinazohitajika za data hizo na kuwa data hizo hazitakiuka wala kuvunja haki zozote za kibinafsi au za kimiliki za wahusika wowote wa kando tena data hizo hazina madhara yoyote (ikiwa ni pamoja na, bali sio tu, virusi vya kompyuta, bomu za kikompyuta, Trojani, minyoo, vitu vya kudhuru, data mbovu au programu nyingine zinazoweza kusababisha madhara au data yenye madhara).

OUP ina haki ya kuamua, bila kuhusisha uamuzi wa mwingine, kurekebisha, kuhariri au kufuta makala yoyote yaliyochapishwa na watumiaji, ambayo OUP inachukulia kuwa hayafuati Miongozo (kiungo) na/au yanamharibia mtu jina, yanakiuka sheria, yanatisha, yana lugha chafu au yanapingika kwa namna moja au nyingine. Licha ya yaliyotajwa hapo juu, OUP inajiondoa kwenye hatia inayotokana na makala yaliyopakiwa nawe au mtumiaji mwingine yeyote wa Tovuti. Pia, tuna haki ya kufichua utambulisho wako kwa watekelezaji sheria au kwa mhusika yeyote wa kando anayedai kwamba makala yoyote uliyoyachapisha au kupakia kwenye Tovuti yetu yanakiuka haki zao za mali ya kiakili, au haki yao ya faragha.


Haki ya OUP ya kutumia makala kutoka kwa mtumizi
Maudhui yoyote upakiayo kwenye Tovuti yetu yatachukuliwa kuwa yasiyo ya siri. Kwa vile OUP imekuruhusu utumie Tovuti hii kulingana na Ilani hii ya Kisheria (angalia Utumiaji wa maudhui ya Tovuti hapo juu), unaipa OUP leseni ya daima, ya ulimwenguni kote, isiyotengulika, isiyo na mirahaba, inayoweza kuhamishika, inayoweza kutumiwa na wengi ya kutumia, kuhariri, kuchanganua, kuchapisha, kuonyesha, kuwasiliana na umma kuyahusu na kuyatumia maradufu makala haya (au sehemu yao yoyote) katika lugha zote katika mfano wowote au chombo chochote kile iwe kipo au hakipo kwa sasa (na kutoa leseni hizi kwa wengine). Unajiondolea haki zozote za kimaadili kwa makala yoyote unayopakia kwenye Tovuti yetu (ikiwa ni pamoja na bali sio tu haki ya kutambuliwa kama mwandishi). Huenda tukupe heko kwa kazi yako lakini unakubali kwamba si lazima tufanye hivyo.


Makadirio
Tuna haki ya kufuatilia machapisho yote kwenye Tovuti kwa chochote kinachokiuka ilani hii ya kisheria na/au Maelekezo; kwa hivyo, machapisho mengine huenda yatumwe kwa makadirio kabla yachapishwe na, kutokana na hayo, huenda yachelewe kuonekana kwenye Tovuti.


Kusimamishwa na Kukomeshwa
Tutaamua, bila kuhusisha uamuzi wa mwengine, ikiwa Miongozo ama ilani hii ya kisheria imekiukwa [kiungo] kupitia utumiaji wako wa Tovuti. Wakati Miongozo ama ilani hii ya kisheria imekiukwa, tunaweza kuchukua hatua zifuatazo jinsi tunavyochukulia kuwa inafaa ikiwemo bali sio tu uzuiaji mtumiaji yeyote bila onyo wala majadiliano, anayekiuka Miongozo ama ilani hii ya kisheria, na tuondoe michango na machapisho yote ya awali.

Ukiukaji wa Miongozo ama ilani hii ya kisheria unaweza kusababisha uondolewaji wa papo hapo wa ufikiaji wako au haki yako ya kutumia Tovuti hii kwa mda mfupi au kabisa.


Hali ya Kimataifa ya Tovuti
Unatambua hali ya kimataifa ya Tovuti hii na kwa hivyo, unakubali kufuata sheria zote za ndani zinazotumika katika eneo lako unapotumia Tovuti.

Maelezo tunayoyachapisha kwenye Tovuti hii huenda yataje huduma na/au bidhaa zinazotolewa ambazo hazijatangazwa wala hazipo nchini mwako. Kutaja huku hakumaanishi kuwa tunanuia kutangaza huduma na/au bidhaa za aina hii nchini mwako.


Lugha
Ilani hii ya kisheria imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Ikiwa Ilani hii ya kisheria imetafsiriwa katika lugha nyingine yoyote, toleo lile la lugha ya Kiingreza ndilo litakalofuatwa.


Sheria Inayosimamia
Unakubali kwamba Ilani hii ya kisheria itasimamiwa kulingana na sheria za na mahakama zilizoko Uingereza na Wales. Licha ya yaliyotajwa hapo juu, hakuna chochote kilichopo kwenye ilani hii ya kisheria kitakachozuia OUP kuandikisha kesi katika mahakama yoyote kwa minajili ya kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji wa haki zake za mali ya kiakili.


Taarifa kuhusu hadhi ya kiumiliki

Oxforddictionaries.com na tanzu zake huenda ijumuishe maneno yenye au yanayodaiwa kuwa na hadhi ya kiumiliki kama alama za biashara au nyingine. Kujumuishwa kwayo hakumaanishi kuwa yamepata kwa madhumuni ya kisheria, hadhi ya kawaida au hadhi isiyo ya kiumiliki wala hadhi yao ya kisheria haijaharibiwa vyovyote vile. Katika hali ambazo wafanyakazi wahariri wana uthibitisho kwamba neno lina hadhi ya umiliki hii huonyeshwa kwenye ingizo la neno hilo lakini huwa hawatoi maoni wala hawadokezi chochote kingine kuhusu hadhi yao ya kisheria kwa kufanya hivi.


Maoni na maelezo mengine yanayopatikana kwenye machapisho na maoni ya blogu ya OxfordWords hayawakilishi maoni au misimamo ya Oxford University Press.