Ufafanuzi wa -bichi katika Kiswahili

-bichi

kivumishi

 • 1

  -sio bivu.

  ‘Papaibichi’

 • 2

  -siopikwa na kuiva vizuri.

  ‘Kiazi kibichi’

 • 3

  -siokauka, -a majimaji.

  ‘Nguo mbichi’

 • 4

  -siopevuka.

  ‘Kijana mbichi’

 • 5

  mwanzo mwanzo.

  ‘Alfajiri mbichi’

Matamshi

-bichi

/bit∫i/