Ufafanuzi wa -kali katika Kiswahili

-kali

kivumishi

 • 1

  -enye ncha iliyochongoka au inayokata sana.

  ‘Kisu kikali’

 • 2

  -lio chungu.

  ‘Dawa kali’
  chungu, kakasi

 • 3

  -enye kuwasha.

  ‘Pilipili -kali’

 • 4

  -enye kuchoma moyo.

  ‘Hisia -kali’

 • 5

  -enye kuleta kiungulia.

  ‘Limau -kali’

 • 6

  -enye kusisimua mwili.

  ‘Baridi -kali’
  ‘Homa -kali’

 • 7

  -siokuwa -pole k.v. mnyama au mtu.

  ‘Mbwa mkali’
  ‘Mwalimu mkali’

 • 8

  -enye kuvutia na kupendwa sana na watu.

  ‘Wycleff Wamala (Ambasada) ametoa albamu -kali inayoitwa ‘Natamani’’

Matamshi

-kali

/kali/