Ufafanuzi wa -ororo katika Kiswahili

-ororo

kivumishi

 • 1

  kinyume cha -gumu.

  ‘Mwili wake ni mwororo’
  laini, teketeke

 • 2

  -sio na nguvu, vishindo wala kelele.

  ‘Waliburudishwa kwa muziki mwororo wa kileo’

Matamshi

-ororo

/ɔrɔrɔ/