Ufafanuzi msingi wa bomu katika Kiswahili

: bomu1bomu2

bomu1

nominoPlural mabomu

 • 1

  silaha iliyotengenezwa kwa vitu vinavyolipuka ambavyo husababisha madhara makubwa mahali inapolipukia.

  ‘Bomu la atomiki’
  ‘Bomu la nyukilia’
  kombora

 • 2

  kombora dogo linalotengenezwa kwa kutumia chupa au kibati.

 • 3

  swali au jambo gumu.

 • 4

  sauti kubwa ya ngoma.

 • 5

  ngoma ndefu yenye sauti nzito.

  ‘Bomu la gogo’

 • 6

  mtindo fulani wa kucheza ngoma mojawapo ya kizamani.

Asili

Kng

Matamshi

bomu

/bɔmu/

Ufafanuzi msingi wa bomu katika Kiswahili

: bomu1bomu2

bomu2

kitenzi elekezi~ana, ~lia, ~lika, ~lisha, ~liwa

 • 1

  angamiza kwa kutumia bomu.

 • 2

  shambulia mtu kwa maneno.

Asili

Kng

Matamshi

bomu

/bɔmu/