Ufafanuzi msingi wa bunda katika Kiswahili

: bunda1bunda2

bunda1

nomino

 • 1

  fungu la vitu kama karatasi au nguo vilivyofungwa pamoja.

  ‘Bunda la noti’
  ‘Bunda la katani’
  ‘Bunda la karatasi’
  furushi, burungutu

Asili

Kng

Matamshi

bunda

/bunda/

Ufafanuzi msingi wa bunda katika Kiswahili

: bunda1bunda2

bunda2

kitenzi elekezi

 • 1

  shindwa mtihani.

  ‘Matokeo yanaonyesha watoto wengi wamebunda mitihani yao’

Matamshi

bunda

/bunda/