Ufafanuzi msingi wa chapa katika Kiswahili

: chapa1chapa2chapa3

chapa1

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  piga kwa kutia adabu au kuumiza.

  ‘Chapa kibao’
  ‘Chapa bakora’
  piga, tandika

 • 2

  funga mtu au timu fulani magoli.

  ‘Timu ya Benki imeichapa timu ya Linare mabao 9–1’

Matamshi

chapa

/t∫apa/

Ufafanuzi msingi wa chapa katika Kiswahili

: chapa1chapa2chapa3

chapa2

nominoPlural chapa

 • 1

  alama ya bidhaa au biashara inayowekwa juu ya kitu kuonyesha kile ni cha mtu fulani au kinakwenda mahali fulani au inayoeleza jambo fulani kuhusu kitu kile.

  rajamu

 • 2

  nakshi, mchoro

Matamshi

chapa

/t∫apa/

Ufafanuzi msingi wa chapa katika Kiswahili

: chapa1chapa2chapa3

chapa3

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  andika herufi juu ya karatasi au mahali fulani kwa kutumia taipu au mitambo.

  ‘Chapa kitabu/gazeti’

Asili

Khi

Matamshi

chapa

/t∫apa/