Ufafanuzi msingi wa china katika Kiswahili

: china1china2

china1

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  kaa kwa muda mrefu kwa kitu k.v. chakula na kuanza kuharibika.

 • 2

  shindwa kupata kilichotamaniwa.

 • 3

  chelewa sana.

  doda, selea

Matamshi

china

/t∫ina/

Ufafanuzi msingi wa china katika Kiswahili

: china1china2

china2

kielezi

 • 1

  (hutumika kuelezea vitendo viwili vinavyofanywa sawia) kwa wakati huohuo.

  ‘Akitabasamu china akilia’

Matamshi

china

/t∫ina/