Ufafanuzi wa chomoa katika Kiswahili

chomoa

kitenzi elekezi~ana, ~ka, ~lea, ~leana, ~lewa, ~za

 • 1

  toa kitu mahali kilipotiwa au kilipopigiliwa.

  ‘Chomoa msumari ukutani’
  ‘Chomoa mwiba mguuni’
  ‘Chomoa upanga’
  komoa

 • 2

  pata kitu kwa ulaghai au udanganyifu.

 • 3

  iba kutoka mfukoni mwa mtu.

Matamshi

chomoa

/t∫ɔmɔwa/