Ufafanuzi wa chuja katika Kiswahili

chuja

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  tenga maji au kitu cha majimaji na kitu ambacho si cha majimaji kwa kutumia chombo chenye matundumatundu au chujio.

  ‘Chuja chai’

 • 2

  ondoa takataka katika maji au kitu cha majimaji.

  chuza

 • 3

  kamua na toa maji katika kitu.

  ‘Chuja nazi’

 • 4

  toweka pamoja na.

 • 5

  tenga ili kuchagua bora kati ya washindani, watahiniwa au waliohojiwa.

Matamshi

chuja

/t∫uʄa/