Ufafanuzi wa deka katika Kiswahili

deka

kitenzi sielekezi~ea, ~eka, ~eza

  • 1

    jipendekeza na jifanya kama mtoto afanyavyo kwa wazazi wake hasa wakati anapotaka kitu.

  • 2

    tia maringo kwa kujivunia ulichonacho; fanya kiburi.

  • 3

    tumaini jambo kwa mtu ambaye una hakika kwamba anaweza kukusaidia.

Matamshi

deka

/dɛka/