Ufafanuzi wa endesha katika Kiswahili

endesha

kitenzi elekezi~ana, ~ea, ~eana, ~eka, ~ewa, ~wa

 • 1

  ongoza chombo cha usafiri k.v. gari au baiskeli kielekee mahali fulani.

 • 2

  peleka mtu kwa gari.

  ‘Juma anamwendesha Meneja Mkuu’

 • 3

  fanyia mtu vitendo vya kumdhalilisha.

 • 4

  harisha.

  ‘Dawa ya kuendesha’
  hara

Matamshi

endesha

/ɛndɛ∫a/