Ufafanuzi wa foka katika Kiswahili

foka

kitenzi sielekezi~ea, ~eana, ~eka, ~esha, ~ewa

 • 1

  kutoa povu kwa maziwa wakati yanapochemka na kutaka kumwagika.

 • 2

  toka maji kwa nguvu k.v. katika chemchemi au tundu katika mashua.

  bubujika, buguika

 • 3

  toa maneno harakaharaka na kwa hasira; sema kwa ukali.

  hamaki

Matamshi

foka

/fɔka/