Ufafanuzi msingi wa funda katika Kiswahili

: funda1funda2funda3

funda1

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa, ~ana

 • 1

  twanga vitu vikavu mpaka viwe laini kama unga.

  ‘Funda makopa’
  ponda, twanga, dunda

Matamshi

funda

/funda/

Ufafanuzi msingi wa funda katika Kiswahili

: funda1funda2funda3

funda2

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa, ~ana

 • 1

  fundisha, hasa mafundisho ya nyumbani.

 • 2

  tia unyagoni.

  lea, funza

Matamshi

funda

/funda/

Ufafanuzi msingi wa funda katika Kiswahili

: funda1funda2funda3

funda3

nominoPlural mafunda

 • 1

  ujazo wa chakula au kinywaji kinywani na kuvimbisha mashavu.

Matamshi

funda

/funda/