Ufafanuzi wa fungua katika Kiswahili

fungua

kitenzi elekezi~ana, ~ka, ~lia, ~liana, ~lisha, ~za, ~liwa

 • 1

  acha wazi k.v. mlango au sanduku.

 • 2

  achia huru k.v. mtu aliyefungwa.

  feleti

 • 3

  legeza kamba ya kitu kilichofungwa.

  ‘Fungua kuni’

 • 4

  anzisha jambo.

  ‘Fungua hospitali’

 • 5

  acha kufunga saumu.

Matamshi

fungua

/funguwa/