Ufafanuzi wa goboa katika Kiswahili

goboa, koboa

kitenzi elekezi~ka, ~lea, ~leana, ~lesha, ~lewa

 • 1

  vunja kwa mkono mhindi kutoka kwenye shina.

 • 2

  safisha k.v. pamba au karafuu kwa kuondoa vikonyo vyake.

 • 3

  kongoa k.v. msumari.

 • 4

  bandua k.v. magome ya miti.

 • 5

  ondoa maganda ya nafaka k.v. mahindi au mpunga.

Matamshi

goboa

/gɔbɔwa/