Ufafanuzi wa hatua katika Kiswahili

hatua

nominoPlural hatua

 • 1

  nafasi kati ya wayo na wayo wa pili wa mtu anayekwenda kwa miguu; kipimo cha mwendo wa miguu.

  ‘Pima kwa hatua’
  ‘Hatua mbili mbele’
  msamba

 • 2

  maendeleo

 • 3

  ‘Nitakuja nikipata hatua’
  nafasi, faragha

 • 4

  tendo linalofaa kufanyiwa jambo fulani.

  ‘Chukua hatua’

Asili

Kar

Matamshi

hatua

/hatuwa/