Ufafanuzi wa iva katika Kiswahili

iva

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  kuwa mbivu; pevuka k.v. matunda.

 • 2

  pikika na kuwa tayari chakula kwa ajili ya kuliwa.

  ‘Nyama imeiva’

 • 3

  kuwa tayari kwa jambo lililokuwa linaandaliwa.

  ‘Mambo yameiva’
  ‘Ona haya’

Matamshi

iva

/Iva/