Ufafanuzi msingi wa jaa katika Kiswahili

: jaa1jaa2

jaa1

kitenzi elekezi~lia, ~lika, ~liwa, ~wa, ~za

 • 1

  kuwa tele.

  ‘Mtungi umejaa maji’

 • 2

  tapakaa kila mahali.

  ‘Nzige walijaa kote’
  enea

 • 3

  kuwa na maungo makubwa.

  nenepa

Matamshi

jaa

/ʄa:/

Ufafanuzi msingi wa jaa katika Kiswahili

: jaa1jaa2

jaa2

nominoPlural majaa

 • 1

  mahali pa kutupia taka.

  jalala

 • 2

  chungu cha taka.

Matamshi

jaa

/ʄa:/