Ufafanuzi wa jenga katika Kiswahili

jenga

kitenzi elekezi~ana, ~ea, ~eka, ~esha, ~wa

 • 1

  simamisha kitu k.v. nyumba, kwa kutumia udongo, chokaa au saruji.

  ‘Jenga shule’

 • 2

  fanya madhubuti.

  ‘Jenga taifa’
  ‘Jenga nchi’
  ‘Jenga mwili’
  ‘Jenga imani’
  imarisha

 • 3

  saidia mtu ili apate kitu k.v. cheo au masilahi makubwa zaidi.

Matamshi

jenga

/ʄɛnga/