Ufafanuzi wa kitamkwa katika Kiswahili

kitamkwa

nominoPlural vitamkwa

Sarufi
 • 1

  Sarufi
  kipande cha sauti kinachofanyizwa na ala za matamshi k.v. meno, ufizi, ulimi, midomo au kaakaa katika mfumo wa matamshi ya lugha.

  ‘P na b ni vitamkwa vya midomoni’

 • 2

  Sarufi
  sauti dhahiri inayosikika wakati wa utamkaji maneno ambayo huweza kuwakilishwa kimaandishi kwa kutumia alfabeti.

Matamshi

kitamkwa

/kitamkwa/