Ufafanuzi wa kwa katika Kiswahili

kwa

kiunganishi

 • 1

  neno linaloweka uhusiano baina ya kitendo na kitu kilichotumiwa kutendea kitendo hicho.

  ‘Alimpiga kwa fimbo’

 • 2

  namna au njia ya kufanyia kitendo fulani.

  ‘Alimwendea kwa siri’

 • 3

  hutumika kuonyesha kuwa mahali fulani kunamhusu mtu fulani.

  ‘Anatoka kwa Ali’
  ‘Nitakwenda kwa kiongozi’
  ‘Unakwenda kwa nani?’

 • 4

  hutumika kuonyesha mshabaha au tofauti.

  ‘Wamefungana mabao matano kwa mawili’

 • 5

  hutumika kuonyesha utumikaji wa kitu pamoja na kitu kingine.

  ‘Alikula wali kwa mchuzi’

Matamshi

kwa

/kwa/