Ufafanuzi wa legea katika Kiswahili

legea

kitenzi sielekezi~za

 • 1

  kuwa laini.

  ‘Ndizi hizi zimelegea’
  tebwereka, tepetea, cheza

 • 2

  kosa kukazika.

  ‘Fundo ulilolifunga limelegea’
  legalega

 • 3

  kuwa tepetevu; kuwa dhaifu; kosa kukazana.

  ‘Mtoto huyu amelegea mno’
  tabwarika

Matamshi

legea

/lɛgɛa/