Ufafanuzi wa mafuta katika Kiswahili

mafuta

nominoPlural mafuta

 • 1

  kiowevu chenye uto kinachotokana na mimea k.v. ufuta, nazi, karanga au kweme.

  ‘Mafuta ya uto’
  ‘Mafuta ya nazi’

 • 2

  madini ya majimaji yanayotumiwa kutengeneza petroli, dizeli au lami.

  ‘Mafuta ya taa’

 • 3

  sehemu ya nyama iliyonona.

  shahamu

Matamshi

mafuta

/mafuta/