Ufafanuzi wa maji katika Kiswahili

maji

nominoPlural maji

 • 1

  kiowevu kinachopatikana kutokana na mvua katika bahari, maziwa, mito, n.k. ambacho hutumika kwa kupikia, kunywa au kuogea.

  methali ‘Maji ya kifuu bahari ya chungu’
  methali ‘Maji ukiyavulia nguo yaoge’
  methali ‘Maji yakijaa, hupwa’
  methali ‘Maji usiyoyafika huyajui wingi wake’
  methali ‘Maji hufuata mkondo’
  methali ‘Maji mafu na mvuvi kafu’
  methali ‘Maji yakimwagika hayazoleki’
  methali ‘Maji ya nazi yatafuta mvugulio’
  methali ‘Maji ya moto hayachomi nyumba’

Matamshi

maji

/maʄi/