Ufafanuzi wa mdundo katika Kiswahili

mdundo

nominoPlural midundo

 • 1

  tendo la kugonga kwa kitu k.v. ngoma.

  ‘Piga ngoma mdundo mmoja’

 • 2

  upigaji wa kitu mahali pagumu ili kirudi au kipae juu.

 • 3

  mtwango wa kitu k.v. katika kinu.

 • 4

  wimbo au muziki.

  ‘Bendi ya Mlimani Park jana ilipiga mdundo mmoja mzuri sana’

Matamshi

mdundo

/mdundɔ/