Ufafanuzi wa mea katika Kiswahili

mea

kitenzi sielekezi

 • 1

  chipuka kwa kitu kilichopandwa ardhini.

  ‘Mbegu uliyopanda imemea’
  ota

 • 2

  tokeza au kua kitu kwenye mwili wa binadamu, mnyama au mdudu.

  ‘Mea mbawa’
  ‘Mea nywele’