Ufafanuzi msingi wa mlango katika Kiswahili

: mlango1mlango2mlango3

mlango1

nomino

 • 1

  uwazi au nafasi maalumu iliyo ukutani ili kuingilia na kutokea mahali au penye uwazi zaidi.

 • 2

  kizuizi kilichotengenezwa kwa ubao, chuma au kitu kingine chochote ili kuziba uwazi wa kuingilia na kutokea kwenye ukuta au kiambaza cha jengo, chumba au gari.

Ufafanuzi msingi wa mlango katika Kiswahili

: mlango1mlango2mlango3

mlango2

nomino

 • 1

  kikundi cha watu wanaotokana na nasaba moja.

  ukoo, uzawa, ufungu

Matamshi

mlango

/mlangÉ”/

Ufafanuzi msingi wa mlango katika Kiswahili

: mlango1mlango2mlango3

mlango3

nomino

 • 1

  sehemu iliyogawanywa katika kitabu.

  sura, babu, faslu

Matamshi

mlango

/mlangÉ”/