Ufafanuzi wa mtu katika Kiswahili

mtu

nominoPlural watu

 • 1

  kiumbe anayetembea wima ambaye hutumia fikira zaidi kuliko silika kufanya mambo yake.

  methali ‘Mtu akivuliwa nguo huotama, hainuki’
  methali ‘Mtu hakatai mwito, hukataa aitiwalo’
  methali ‘Mtu hujikuna ajipatapo’
  methali ‘Mtu huulizwa amevaani, haulizwi amekulani’
  methali ‘Mtu ni watu’
  methali ‘Mtu pweke ni uvundo’
  mwanadamu, mahuluku, binadamu

Matamshi

mtu

/mtu/