Ufafanuzi wa mvulana katika Kiswahili

mvulana

nominoPlural wavulana

 • 1

  mtoto wa kiume.

  ghulamu

 • 2

  kijana wa kiume aliyekwisha kubaleghe na ambaye hajafikia umri wa miaka kama thelathini na tano hivi.

  mvuli

 • 3

  kijana wa kiume ambaye ni mpenzi wa mwanamke fulani.

  ‘Yohana ni mvulana wa Roza’

Matamshi

mvulana

/mvulana/