Ufafanuzi wa mwenyeji katika Kiswahili

mwenyeji

nominoPlural wenyeji

  • 1

    mtu ambaye amezaliwa mahali fulani na akaendelea kukaa hapo.

  • 2

    mtu mwenye maskani yake mahali fulani hata kama hakuzaliwa hapo.

  • 3

    mtu au ofisa wa nchi au taasisi anayepokea na kuwahudumia wageni wa k.v. mkutano, warsha, kongamano au michezo.

Matamshi

mwenyeji

/mwɛɲɛʄi/