Ufafanuzi wa nyegere katika Kiswahili

nyegere

nominoPlural nyegere

  • 1

    mnyama mdogo mwenye kichwa kikubwa na masikio madogo ya mviringo mwenye rangi nyeusi mwilini, nyeupe au kijivu mgongoni, mkia wake ni mfupi wenye manyoya mengi, hupenda kula asali na mwenye ushuzi unaowalevya nyuki katika mzinga.

    ‘Anapenda asali kama nyegere’

Matamshi

nyegere

/ɲɛgɛrɛ/