Ufafanuzi wa pasua katika Kiswahili

pasua

kitenzi elekezi~ana, ~ka, ~lia, ~liana, ~lisha, ~liwa

 • 1

  fanya kitu kuwa mbale au vipande.

  ‘Pasua mbao’
  banja

 • 2

  fanya kitu kuacha kushikana.

  ‘Pasua nguo’
  ‘Pasua karatasi’
  vunja, tema, chanja, chana, rarua

 • 3

  fanya kitu kuwa na jeraha au kidonda.

  ‘Alimpiga kwa jiwe akampasua’

 • 4

  ‘Pasua nywele’
  tenganisha

Matamshi

pasua

/pasuwa/