Ufafanuzi wa pekecha katika Kiswahili

pekecha

kitenzi elekezi~ea, ~eana, ~eka, ~esha, ~ewa, ~wa

 • 1

  zungushazungusha kitu k.v. kijiti katikati ya viganja vya mikono vilivyoshikamana ili kuwasha moto au kutoboa tundu.

 • 2

  toboa tundu au chimba shimo kwa kutumia chombo kinachozunguka wakati wa kuchimba.

 • 3

  kufanya kitu k.v. uji kiwe laini.

 • 4

  kitendo cha mdudu kutoboa mti hasa mkavu au nafaka.

Matamshi

pekecha

/pɛkɛtʃa/