Ufafanuzi wa penya katika Kiswahili

penya

kitenzi elekezi~ea, ~eana, ~eka, ~ewa, ~eza, ~wa

 • 1

  pita kwenye tundu dogo, ufa au mwanya finyu kwa kujigagamiza.

  ingia

 • 2

  pita kwa kufanya tundu katika kitu.

  ‘Risasi imepenya ukutani’
  bokoa

 • 3

  ingia ndani ya moyo au fikira.

  ‘Mawaidha yake yamempenya kila mtu’

Matamshi

penya

/pɛɲa/