Ufafanuzi wa pita katika Kiswahili

pita

kitenzi sielekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  endelea na mwendo kwa kufuata njia ili kufika mahali fulani.

 • 2

  kuwa -a zamani; kuwa -a wakati wa nyuma.

  ‘Mambo haya yamepita, hakuna haja ya kuyazungumza’

 • 3

  kuwa -a kutodumu.

  ‘Mitindo ya nguo ni mambo ya kupita , kila wakati huja na mtindo wake’

 • 4

  kuwa zaidi ya.

  ‘Amenipita kwa urefu’
  zidi, shinda, fyokocha, kulula, fora

Matamshi

pita

/pita/