Ufafanuzi msingi wa pua katika Kiswahili

: pua1pua2pua3pua4

pua1

nomino

 • 1

  kiungo cha mwili wa kiumbe, chenye tundu, kilicho juu ya mdomo na kinachomwezesha kuvuta pumzi na kunusia.

Matamshi

pua

/puwa/

Ufafanuzi msingi wa pua katika Kiswahili

: pua1pua2pua3pua4

pua2

nomino

 • 1

  sehemu ya tanga inayoweza kukunjwa.

Matamshi

pua

/puwa/

Ufafanuzi msingi wa pua katika Kiswahili

: pua1pua2pua3pua4

pua3

kitenzi elekezi

 • 1

  paka kitu kiowevu k.v. mafuta mwilini kwa kutandaza kiganja cha mkono.

  ‘Anajipua dawa mwilini’

Matamshi

pua

/puwa/

Ufafanuzi msingi wa pua katika Kiswahili

: pua1pua2pua3pua4

pua4

kitenzi elekezi

 • 1

  maliza yote bila ya kubakisha kitu.

  ‘Amepua wali’

Matamshi

pua

/puwa/