Ufafanuzi wa sababu katika Kiswahili

sababu

nominoPlural sababu

 • 1

  kitu kinachofanya kitu kingine kitokee.

  ‘Hebu nieleze sababu ya mwalimu kukuadhibu’
  kisa, mwanzo, maana, kasidi, chanzo

 • 2

  maelezo yanayoonyesha kwa nini hoja zilizotolewa hazikubaliki.

  ‘Toa sababu zako za kutokubaliana naye’

 • 3

  lengo au madhumuni yanayompeleka mtu kufanya jambo fulani.

  ‘Nimekuja hapa kwa sababu yako’
  ili, ajili

Asili

Kar

Matamshi

sababu

/sababu/