Ufafanuzi msingi wa sega katika Kiswahili

: sega1sega2

sega1

nominoPlural masega

 • 1

  jengo la nta lililotengenezwa na nyuki lenye vijumba vingi ambavyo nyuki huwekea asali na watoto wao.

  zana, kitata

Matamshi

sega

/sɛga/

Ufafanuzi msingi wa sega katika Kiswahili

: sega1sega2

sega2

kitenzi elekezi~ea, ~eana, ~eka, ~esha, ~ewa, ~wa

 • 1

  pandisha au kunja nguo k.v. suruali au shuka, hadi kufikia magotini ili isipate maji, isichafuke, n.k..

  ‘Sega nguo’
  pania

Matamshi

sega

/sɛga/