Ufafanuzi msingi wa sheria katika Kiswahili

: sheria1sheria2

sheria1

nominoPlural sheria

 • 1

  kanuni zinazotungwa na bunge la nchi fulani ili kusimamia taratibu za nchi hiyo na ambazo ni lazima zifuatwe na watu waliomo humo na anayekwenda kinyume nazo hupewa adhabu na mahakama.

 • 2

  kanuni zinazotungwa na chombo k.v. halmashauri kilichopewa mamlaka na bunge ili kusimamia taratibu za mahali fulani k.v. mji, kampuni au shirika.

  ‘Kawaida ni kama sheria’
  ‘Sheria haina kwao’
  methali ‘Sheria ni msumeno’

Ufafanuzi msingi wa sheria katika Kiswahili

: sheria1sheria2

sheria2 , sharia

nominoPlural sheria

Kidini
 • 1

  Kidini
  kanuni zinazoendesha taratibu za maisha ya waumini wa dini fulani na ambazo zinasadikiwa zinatoka kwa Mwenyezi Mungu.

Asili

Kar

Matamshi

sheria

/∫ɛrija/