Ufafanuzi wa shtua katika Kiswahili

shtua, shitua, stua

kitenzi elekezi~ana, ~ka, ~lia, ~liwa, ~sha

 • 1

  fanyia mtu, mnyama, ndege, n.k. kitendo cha kumtaharukisha kwa ghafla k.v. kupiga kelele, kutikisa au kugonga kitu.

  ‘Nilimshtua ndege, akaruka’
  kurupusha, gutua, goga, kurupua, tisha

 • 2

  fanya kitu k.v. kiungo cha mwili kuondoka mahali pake.

  ‘Amempiga mwenzake teke mpaka amemshtua goti’

Matamshi

shtua

/∫tuwa/