Ufafanuzi wa siasa katika Kiswahili

siasa

nominoPlural siasa

 • 1

  itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima wa maisha ya jamii hiyo.

  ‘Siasa ya ubepari’
  ‘Siasa ya ubaguzi wa rangi’
  ‘Elimu ya siasa’

 • 2

  mbinu ya utekelezaji au uendeshaji wa jambo kwa kutumia busara na hekima ili kufikia lengo linalotarajiwa.

  ‘Fanya mambo kwa siasa’
  ‘Hutaweza kufaulu katika jambo hili mpaka utumie siasa’

Asili

Kar

Matamshi

siasa

/sijasa/