Ufafanuzi msingi wa siri katika Kiswahili

: siri1siri2

siri1

nominoPlural siri

  • 1

    habari au jambo lililofichwa.

    hombo, faragha, fumbo, kificho, choza

Asili

Kar

Matamshi

siri

/siri/

Ufafanuzi msingi wa siri katika Kiswahili

: siri1siri2

siri2

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

  • 1

    geuka kwa jambo au mambo na kuwa katika hali nyingine.

    ‘Walikuwa wakipigania nyumba ile, lakini kulipotolewa ushahidi ikasiri kuwa wote wawili si yao’

Asili

Kar

Matamshi

siri

/siri/