Ufafanuzi msingi wa sura katika Kiswahili

: sura1sura2sura3

sura1

nominoPlural sura

 • 1

  umbile k.v. la mtu au mnyama lililoko usoni.

  kifani, dutu

 • 2

  namna au jinsi ya kitu.

  ‘Jambo hili linaweza kufanyika katika sura mbalimbali’

 • 3

  hali ya mtu inayojitokeza usoni k.v. baada ya kufikwa na jambo.

  ‘Sura yake haikuonyesha kuwa ana msiba’

Asili

Kar

Matamshi

sura

/sura/

Ufafanuzi msingi wa sura katika Kiswahili

: sura1sura2sura3

sura2

nominoPlural sura

 • 1

  sehemu katika kitabu iliyogawanywa, agh. kutokana na muktadha.

  mlango, faslu

Matamshi

sura

/sura/

Ufafanuzi msingi wa sura katika Kiswahili

: sura1sura2sura3

sura3

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

Matamshi

sura

/sura/