Ufafanuzi wa tetereka katika Kiswahili

tetereka

kitenzi sielekezi~ea, ~eka, ~esha

 • 1

  enda upandeupande au kwa kupepesuka.

 • 2

  poteza mwelekeo au msimamo uliokuwepo awali.

  ‘Ushirikiano wao umeanza kutetereka’

 • 3

  kuwa kando kidogo ya pahali panapotakiwa au pa kawaida.

  ‘Alianguka na mguu wake ukatetereka kidogo lakini haukuvunjika’
  fusika

Matamshi

tetereka

/tɛtɛrɛka/