Ufafanuzi msingi wa tupu katika Kiswahili

: tupu1tupu2tupu3

tupu1

kivumishi

 • 1

  -siyo na kitu ndani.

  ‘Chupa tupu’
  kichele, -eupe

 • 2

  bila ya kitu kingine zaidi.

  ‘Waliohudhuria ni wanawake wa tupu’
  ‘Wali mtupu’

Matamshi

tupu

/tupu/

Ufafanuzi msingi wa tupu katika Kiswahili

: tupu1tupu2tupu3

tupu2

kielezi

 • 1

  bila ya kuvaa au kujifunika nguo.

  chini, uchi

Matamshi

tupu

/tupu/

Ufafanuzi msingi wa tupu katika Kiswahili

: tupu1tupu2tupu3

tupu3

nominoPlural tupu

 • 1

  kiungo cha binadamu k.v. kuma, mboo na mkundu, kinachotumiwa kwa k.v. kunyea na kukojolea.

Matamshi

tupu

/tupu/