Ufafanuzi msingi wa umua katika Kiswahili

: umua1umua2umua3

umua1

kitenzi elekezi~ka, ~lia, ~liwa, ~sha, ~ana, ~liana, ~lika, ~lisha

 • 1

  changanya unga, agh. wa ngano, pamoja na vitu vyenye uchachu au hamira na maji ili ufure.

Matamshi

umua

/umuwa/

Ufafanuzi msingi wa umua katika Kiswahili

: umua1umua2umua3

umua2

kitenzi elekezi~ka, ~lia, ~liwa, ~sha, ~ana, ~liana, ~lika, ~lisha

 • 1

  nyang’anya, pokonya au torosha mke kutoka kwa mume wake.

 • 2

  nyang’anya nyuki asali yake.

Matamshi

umua

/umuwa/

Ufafanuzi msingi wa umua katika Kiswahili

: umua1umua2umua3

umua3

kitenzi elekezi~ka, ~lia, ~liwa, ~sha, ~ana, ~liana, ~lika, ~lisha

 • 1

  tia madini yaliyoyeyuka katika kitu ili yakipoa na kuganda yachukue umbo la kile kitu.

Matamshi

umua

/umuwa/