Kuhusu OGLMnamo mwaka wa 2015 Oxford Dictionaries ilizindua mpango mpya wa dijitali unaosisimua wa lugha za kimataifa kama sehemu ya kazi yake ya kueneza mafunzo na elimu kote ulimwenguni.


Je, Oxford Global Languages ni nini, na lugha gani zitajumuishwa?

Oxford Global Languages (OGL) ni mradi mkubwa kutoka OUP wa kuunda  raslimali za kileksikografia za lugha 100 za ulimwengu na kuzifanya zipatikane mtandaoni. Kwa mara ya kwanza, viwango vikubwa vya maelezo bora kuhusu misamiati ya lugha nyingi vitaundwa, kukusanywa na kupatikana kwa urahisi na kwenye mpangilio maalum kwa wazungumzaji, wanafunzi na watengenezaji kupitia hifadhi inayofikiwa kwa kiungo kimoja. Lengo la mradi huu ni kubadilisha mazoea ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni kwa kufanya makala yaliyo katika lugha yao yapatikane katika mfumo wa dijitali, kwenye Tovuti, programu, na katika vifaa na huduma mbalimbali. 


Mpango wa OGL utasaidia:

  • Kukusanya maudhui yanayohusiana na lugha hai, ikiwa ni pamoja na lahaja na sajili zao, na kurekodi kwa hakika jinsi yanavyotumiwa leo hii
  • Kuongeza ufikiaji wa kimataifa wa raslimali za lugha kwa kujenga hifadhi kubwa ya data ya kuhifadhi data ya lugha inayofikika, iliyoungana, na inayoweza kutumika tena na tena 
  • Kuwezesha utengenezaji wa vifaa na raslimali mpya za dijitali kwa minajili ya kuimarisha na kusaidia lugha za kimataifa 
  • Kuongeza ufahamu na ujuzi wa jamii kuhusu lugha kote ulimwenguni

Oxford Global Languages ilizindua tovuti zake mbili za kwanza za lugha, isiZulu na Sotho ya Kaskazini, katika mwaka wa 2015. Malay, Urdu, Setswana, na Kiindonesia zimefuata, na nyinginezo nyingi pia zitaongezwa katika miaka kadhaa ijayo.

Angalia orodha kamili ya lugha zilizoko katika mpango wa OGL >>