Ufafanuzi wa -gumu katika Kiswahili

-gumu

kivumishi

 • 1

  -sio laini au -ororo.

  ‘Chuma ni kigumu’
  kavu, jamidi, kaukau

 • 2

  -sio -epesi kueleweka.

  ‘Hesabu hizi ni ngumu’

 • 3

  -enye moyo shupavu; -siokuwa na huruma.

  ‘Ana moyo mgumu’
  kakamizi

 • 4

  bahili

Matamshi

-gumu

/gumu/