Ufafanuzi msingi wa bandika katika Kiswahili

: bandika1bandika2

bandika1

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iza, ~iwa, ~wa

 • 1

  shikamanisha kwa gundi au kwa pini au kitu kingine kinachonata.

  ‘Bandika stempu’

 • 2

  weka kitu juu ya kingine.

  ‘Bandika mtungi kichwani’
  ‘Bandika chungu motoni’
  ‘Bandika dawa’
  twika

 • 3

  ambatana na mtu bila ya kumwacha.

  ‘Amejibandika kwa fulani’

Matamshi

bandika

/bandika/

Ufafanuzi msingi wa bandika katika Kiswahili

: bandika1bandika2

bandika2

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iza, ~iwa, ~wa

 • 1

  nunua kitu kwa kulipa kidogokidogo, agh. dukani, hadi malipo yanapomalizika.

  ‘Wanawake wengi hubandika kanga’

Matamshi

bandika

/bandika/